Kitanda cha Kulalia Mgonjwa
1.Utangulizi
Kubuni na kutengeneza vifaa vya matibabu kwa ajili ya utoaji tiba kwa kwenye taasisi za afya lilibuniwa na Taasisi ya Uhandisi na Usanifu Mitambo (TEMDO) likiwa na lengo la kuwezesha nchi kuweza kujitegemea katika uzalishaji wa vifaa hivyo nchini.
Madhumuni ya mradi huu ni kubuni, na kuzalisha vifaa tiba kwa ajili ya matumizi ya hospitali kwa lengo la kuwezesha nchi yetu kujitegemea katika utengenezaji wa bidhaa hizi. Katika miaka mitano iliyopita, Serikali ya Tanzania imeongeza kwa kiasi kikubwa uwekezaji katika miundombinu ya sekta ya Afya kwa kujenga hospitali na vituo vya afya vipya. Zaidi ya vituo 70 vya kutoa huduma za Afya vimejengwa kote nchini. Ongezeko hili limesababisha ongezeko la mahitaji ya vifaa tiba kwa ajili kuwezesha utoaji wa huduma za afya kwa urahisi na ufanisi.
Ikumbukwe kuwa hivi sasa zaidi ya asilimia 80 ya vifaa tiba nchini vinaagizwa kutoka nje ya nchi (kwa mujibu MSD) kutokana na ukosefu wa uwezo wa utengenezaji na teknolojia miongoni mwa taasisi za ndani. Kwa hivyo, TEMDO kujihusisha na ubunifu na utengenezai wa vifaa hivi kutachochea ubunifu na uzalishaji wa ndani wa vifaa hivi na hivyo basi kuokoa kiasi kikubwa cha fedha za kigeni zinazotumika kuagiza vifaa hivi toka nje ya nchi pamoja na kukuza ujuzi miongoni mwa taasisi za hapa nchini.
2.Umuhimu wa Utengenezaji wa Vifaa Tiba Nchini
Vifaa tiba vinarejelea seti ya vitu vya kawaida vinavyotumiwa kutoa huduma za matibabu ya kina kwa wagonjwa. Vitu hivi ni muhimu katika kutoa huduma kamili za Afya. Katika miaka mitano iliyopita, serikali imezidi kutoa kipaumbele katika kuboresha na kupanua huduma za afya nchini. Kwa hiyo kuna ongezeko kubwa la mahitaji ya vifaa tiba kwa ajili ya hospitali na vituo vya afya vilivyojengwa hivi karibuni na vya zamani.
Kwa sasa, Tanzania inaagiza toka nje ya nchi zaidi ya asilimia 80 ya mahitaji yake ya vifaa tiba. Hali hii imesabishwa na sababu mbali mbali ikiwemo uwekezaji mdogo wa serikali pamoja na sekta binafsi katika ubunifu na utengenezaji wa vifaa tiba. Ni ukweli kwamba tangu nchi yetu imepata uhuru hatujaweza kuwa na taasisi ya serikali au binafsi ambayo ni mahsusi kwa ajili ya utengenezaji wa vifaa tiba licha ya kuwa vifaa tiba ni hitaji la muhimu kwa utoaji wa huduma bora za afya nchini. Kutokana na idadi kubwa ya watu na uwekezaji mkubwa na wa kisasa unaofanyika kwenye sekta ya afya nchini, soko la vifaa tiba nchini ni miongoni mwa masoko kumi makubwa zaidi katika Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara.
Kwa sasa, watengenezaji wengi wa vifaa tiba nchini wanajihusisha zaidi na utengenezaji wa bidhaa za hali ya chini kama vile machela, vitanda vya wagonjwa, vitanda vya kufanyia uchunguzi, skrini n.k. Wazalishaji hawa wa ndani wanakumbana na ugumu wa kufikia viwango vinavyotakiwa kutokana na ushindani mkubwa wa bidhaa kutoka nje, ukosefu wa ujuzi na mitaji. Kwa hiyo, mojawapo ya sababu ya jitihada za TEMDO za kuhimiza ubunifu na uundaji wa vifaa tiba nchini ni kuwezesha nchi kujitegemea katika ushalishaji wa vifaa tiba, kukuza ujuzi na kupunguza gharama ya matumizi ya fedha za kigeni ambazo nchi inalazimika kutumia kuagiza bidhaa ambazo zinaweza kuzalishwa na wazalishaji wa ndani.
3.Mafaniko Yaliyopatikana Hadi Sasa
Ili kuhakikisha TEMDO inafanikiwa katika lengo la kuzalisha vifaa tiba nchini imechukua hatua mbali mbali ikiwemo kuwashirikisha wadau muhimu na mamlaka zinazohusika na kusimamia ubora wa vifaa tiba nchini. Miongoni mwa mafanikio yaliyopatikana ni kuweza kupata cheti cha ithibati kinachoruhusu karakana ya TEMDO kutumika kwa uzalishaji wa vifaa tiba pamoja nakutambua bidhaa za vifaa tiba zinazotengenezwa na TEMDO kuwa zenye ubora na vifango vinavyokubalika. Hatua nyingine ni kupitishwa kwa bidhaa za vifaa tiba zinazotengezwa na TEMDO ambapo hadi sasa bidhaa zilizopitishwa kwa matumizi nchini ni pamoja na:
- i.Drip stand
- ii.Hospital normal bed
- iii.Hospital examination bed
- iv.Delivery bed
- v.Hospital screen
- vi.Bed Side Locker
Zaidi ya vifaa tiba Zaidi ya kumi na moja vimesha buniwa na kusanifiwa, kwasasa utengenezaji wake hauja anza, aidha, ili kuhakikisha Taasisi inakuwa na uwezo wa kuzalisha bidhaa hizi kwa wingi, maboresho yamefanyika kwa kununua mashine za kisasa za karakana za kufanya uzalishaji mkubwa wa vifaa tiba. Picha zilizopo hapa chini zinaonesha baadhi ya bidhaa za vifaa tiba zilizoidhinishwa na taasisi ya udhibiti madawa na vifaa tiba nchini (TMDA) ambazo tayari zinazalishwa na TEMDO.
General Descriptions
Frame work of strong & precise furniture
pipes mounted on rubber.
Two section top of uniformly perforated
Mild steel (MS)sheet.
Backrest section maneuvered by slotted
bar ratchet like mechanism from head end.
Tabular head and foot bows of unequal
height with vertical tube support.
Overall dimension: 1960L x 950W x 600H.
Finish: Painted. capacity: 128kg.