Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara

TEMDO imebuni na kuendeleza mitambo na mashine zaidi ya ishirini (20)

 • 1)Mashine ya kukamua mafuta ya alizeti na mbegu nyingine za mafuta
 • 2)Teknolojia ya kusindika matunda
 • 3)Teknolojia ya kusindika asali na bidhaa za asali
 • 4)Mashine za kupukuchua mahindi.
 • 5)Mashine za kusindika maziwa.
 • 6)Mtambo wa kutengeneza vyakula vya mifugo.
 • 7)Mtambo wa kukamua na kusindika mafuta yatokanayo na michikichi (mawese na mise).
 • 8)Teknolojia ya kutengeneza mkaa unaotokana na vumbi la mbao na mabaki ya mimea
 • 9) Mtambo wa kuchoma taka za hospitalini (Hospital waste incinerator).
 • 10)Mashine ya kuweka dawa kwenye mbegu (Seed dressing equipment)
 • 11)Mtambo wa kutengeneza matofali ya udongo (Clay bricks/ tiles extruding machine)
 • 12)Mtambo wa kuzalisha umeme kwa kutumia upepo
 • 13)Mtambo wa kuchakata bidhaa za Ngozi
 • 14)Machine ya kutoa mbegu kwenye nyanya

Shirika la Uhandisi na Usanifu Mitambo Tanzania (TEMDO), ni mojawapo ya Taasisi zamsingi zilizoanzishwa kwa ajili ya maendeleo ya sekta ya uzalishaji viwandani. Wazo la kuanzisha TEMDO lilijitokeza wakati wa utayarishaji wa mpango wa tatu wa maendeleo wa miaka mitano (1975/76-1979/80), ambapo mkazo mkubwa uliwekwa katika uanzishaji wa viwanda vya msingi (Basic Industries Starategy - BIS). Wakati huo pia ilibainika kuwa kungekuwa na upungufu mkubwa katika utekelezaji wa mpango huo iwapo taifa halitajenga uwezo (Industrial Support Organizations – ISO’s) katika kubuni, kusanifu na kuunda mashine na mitambo kwa ajili ya sekta mbalimbali za uchumi wa nchi.

Serikali ilianzisha Taasisi ya TEMDO kwa Sheria ya Bunge Namba 23 ya mwaka 1980, ili kujenga uwezo katika kubuni, kusanifu na kuunda mitambo na mashine na kuhamasisha utengenezaji wa mashine na mitambo hiyo kibiashara na matumizi yake katika sekta mbalimbali za uchumi wa nchi. TEMDO inahusika vilevile na kutoa huduma za kihandisi katika viwanda na pia kutoa mafunzo kwa mafundi na wahandisi walioko viwandani ili kuongeza tija na weledi, kupelekea uboreshaji wa utendaji kazi na uzalishaji.