Historia

Serikali ilianzisha Taasisi ya TEMDO ili kujenga uwezo katika kubuni, kusanifu na kuunda mitambo na mashine na kuhamasisha utengenezaji kibiashara na matumizi yake katika sekta mbalimbali za uchumi wa nchi. TEMDO inashughulika vilevile na utoaji wa huduma za kihandisi katika viwanda.

Serikali ilianzisha Taasisi ya Uhandisi na Usanifu Mitambo Tanzania (TEMDO) kwa mujibu wa Sheria ya Bunge Na. 23 ya mwaka 1980.

TEMDO inaendesha shughuli zake chini ya Wizara ya Viwanda, Biashara na Masoko na ipo Njiro-Arusha.