Dira, Dhima and Majukumu ya Taasisi
Dira
Dira ya TEMDO ni kuwa mtoa huduma wa rufaa katika kutoa majibu ya kihandisi yanayoongozwa na thamani kwa viwanda vidogo, vya kati na vikubwa kufikia uchumi wa viwanda.
Dhima
Dhima ya TEMDO ni kutoa bidhaa na huduma za kihandisi zenye ubora wa viwango vya juu kwa watengenezaji wadogo na wa kati kwa njia ya kutafiti, kubuni, kuendeleza tekinolojia na kuhawilishaji ili kufikia maendeleo ya viwanda kitaifa.
Majukumu Makuu ya TEMDO
Kulingana na sheria ya Bunge Namba 23 ya mwaka 1980, TEMDO ilipewa kutekeleza majumkumu muhimu yafuatayo:
(i) Kutafiti, kubuni, kuendeleza na kuunda mitambo, mashine na vifaa pamoja na teknolojia mbalimbali, na kuhamasisha utengenezaji wake kibiashara na matumizi yake katika shughuli za uzalishaji mali ili kukuza uchumi;
(ii) Kutoa huduma za kihandisi kwenye viwanda, vidogo, vya kati na vikubwa kwa lengo la kuongeza ufanisi, matumizi bora ya rasilimali, ubora wa bidhaa na uwezo wa ushindani;
(iii) Kutoa mafunzo kwa wahandisi na mafundi mchundo wanaofanya kazi viwandani na taasisi nyingine ili kuongeza ufanisi katika utendaji kazi na uzalishaji mali.