Habari

Imewekwa: Mar, 15 2024

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda,Biashara,Kilimo na Mifugo yafanya ziara TEMDO.

News Images

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda,Biashara,Kilimo na Mifugo yafanya ziara TEMDO.

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara, Kilimo na Mifugo Mhe. Deudatus Mwanyika tarehe 12 Machi, 2024 jijini Arusha akiwa na Waheshimiwa wajumbe wametembelea na kukagua Karakana ya TEMDO (Taasisi ya Uhandisi na Usanifu wa Mitambo Tanzania) ili kujionea teknolojia zinazotengenezwa katika karakana hiyo.

Wakiwa TEMDO Kamati imepongeza karakana hiyo kwa ubunifu wao wa utengenezaji wa vifaa mbali mbali vikiwemo vitanda kwa ajili ya wagonjwa, vitanda vya wakinamama wakati wa kujifungua, majokofu ya kuhifadhia maiti, mashine za kusindika asali, mashine za kusindika karanga pamoja na nyingine nyingi.

Hata hivyo, Mwenyekiti ameendelea kumpongeza Mhe. Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Ashatu Kijaji (Mb) kwa kazi nzuri inayoendelea kufanywa na karakana hiyo. Mhe. Mwenyekiti aliendelea kusema kuwa ni dhahiri sasa watanzania watanufaika na vifaa pamoja na mashine zinazotengenezwa nchini Tanzania hususani katika karakana hiyo.

Aidha, Mhe. Mwenyekiti pamoja na Waheshimiwa wajumbe waliwapongeza sana wajasiriamali ambao wamenufaika na mashine zinazotengenezwa katika karakana hiyo ambazo ni nzuri na gharama nafuu.

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda,Biashara,Kilimo na Mifugo yafanya ziara TEMDO.