Habari
Imewekwa:
Nov, 07 2024
Wanafunzi wa Shule ya msingi NOTRE DAME watembelea TEMDO

Wanafunzi wa Shule ya msingi NOTRE DAME iliyopo jijini Arusha pamoja na walimu wao wametembelea Taasisi ya Uhandisi na Usanifu Mitambo Tanzania (TEMDO) kwa ajili ya kujifunza na kujionea shughuli na kazi mbalimbali zinazofanywa na Taasisi hiyo, leo tarehe 06/11/2024.
Taasisi ya TEMDO imekuwa ikipokea wanafunzi kutoka shule na vyuo mbalimbali na watu wa makundi tofauti tofauti kuja kutembelea ,kujionea na kujifunza tekinolojia ambazo zinazalishwa na Taasisi ya TEMDO kama vile mashine za wajasiliamali, vifaa tiba pamoja na nitambo mengine.