Habari
Ziara ya Baraza la Madiwani Pamoja na Menejimenti ya Halimashauri ya Wilaya ya Nyang’wale - Mkoa wa Geita
Ziara ya Baraza la Madiwani Pamoja na Menejimenti ya Halimashauri ya Wilaya ya Nyang’wale, Mkoa wa Geita waliofanya TEMDO kwa ajili ya kuona na kujifunza Teknolojia mbalimbali zilizozalishwa katika Sekta ya Afya, Kilimo, Ufugaji, Nishati, Uvuvi na Madini.
Maazimio yalio Fanyika
(1) Halmashauri ya Wilaya ya Nyang’wale waliomba TEMDO kufanya ziara ya kikazi katika Halmashauri yao ili iweze kuona fursa na kutatua changamoto zilizopo hususani kwenye sekta ya Madini,Kilimo na Mifugo;
(2) Halmashauri iliazimia kununua Vifaa Tiba vya hospitali moja kwa moja kutoka TEMDO.
(3) TEMDO ijitangaze Zaidi ili watu wengi Zaidi waweze kuifahamu na kufahamu shughuli muhimu zinazofanyika.
(4) TEMDO ijiandae kupokea oda nyingi za mashine za kukoboa na ku "grade" mpunga.
(5) Halmashauri iliomba kupata orodha ya mashine na mitambo Pamoja na bei zake. Orodha hiyo itumwe kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ambae atawafikishia Madiwani wote.