Habari

Imewekwa: Aug, 04 2022

TEMDO ya Ng'ara Maonesho ya Nane Nane Kanda ya Kaskazini

News Images

Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Masoko Dkt. Sigisbert Mmasi akielezea Tecknolojia zilizo buniwa, Kusanifu na Kutengenezwa na TEMDO kwenye kipindi Maalumu kilicho andaliwa na Radio ya TBC Arusha kwaajili ya Maonesho ya Nane Nane. Mitambo iliyo letwa kwenye maonesho hayo ni Kiwanda cha kuchakata Mafuta ya Alizeti, Kiwanda cha Kutengeneza Siagi ya Karanga, Kiwanda cha kuchakata Unga wa Lishe na viungo vya Kupikia, Kiwanda cha kuchakata zao la Muhogo na Sukari. Pia TEMDO ina tengeneza Vifaa Tiba kama vile Vitanda vya kujifungulia wa Mama Wajawazito, Vitanda vya kukagulia na Kulazia Wagonjwa na n.k. Dkt. Mmasi alisema TEMDO ina buni na kutengeneza Mashine na Mitambo Mbali Mbali ikiwemo Majokofu ya kuifadhia maiiti na Kiteketezi cha kuchoma taka hatarishi za hospitali.