Habari

Imewekwa: Jun, 02 2022

TEMDO ni Taasisi "Silaa/Muhimu" katika maendeleo ya Viwanda nchini

News Images

Waziri wa Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara Mhe. Dkt. Ashatu K. Kijaji na Naibu Katibu Mkuu (Dkt. Hashil T. Abdullah) wakipata maelezo ya Mtambo wa Kukamua na kusafisha mafuta ya Alizeti ( Sunflower Oil Processing Plant), Mtambo wa kuchata Sukari ( Small Scale Sugar Processing Plant), Mtambo wa kuchakata zao la Muhogo ( Cassava Processing Plant) na Mtambo wa kuchoma taka hatarishi za hospitali (Bio Medical Hospital Waste Incinerator) walipo tembelea Karakana ya TEMDO. Pia Mhe. Waziri aliweza kujionea Mashine nyingine zinazo tengenezwa na TEMDO kama vile Mashine ya kuchakata zao Mkonge na Karanga, Majokofu ya kuifadhia Maiti, Vifaa Tiba vya hospitali, n.k. Mhe. Waziri ameipongeza TEMDO kwa kanzi nzuri ya Kubuni na Kusanifu Mitambo na Mashine kwaaji ya kuwezesha Sekta ya Viwanda na kupunguza uagizaji wa mitambo, mashine na vifaa nje ya Nchi. Mhe. Waziri alimalizia kwa kusema TEMDO ni Taasisi "Silaa/Muhimu" katika maendeleo ya Viwanda nchin, Kazi Iendelee.