Habari

Imewekwa: May, 27 2020

Waziri ya Viwanda na Biashara Mh. Innocent Bashungwa, azindua mashine mpya TEMDO.

News Images

Waziri wa Viwanda Azindua Mashine Mpya TEMDO.

Waziri wa Viwanda na Biashara Mh. Innocent Bashungwa amemuagiza Mkurugezi mkuu wa Taasisi ya Uhandisi na Usanifu wa Mitambo Tanzania (TEMDO) Eng. Prof. Frederick Kahimba kutengeneza mashine ndogo za kukamua miwa ili kutengeneza Sukari ambayo itawasaidia wazalishaji wadogo na kati kuanza kuzalisha sukari itakayosaidia nchi kuwa na utoshelevu wa mahitaji ndani ya sukari ili kufika malengo mwaka 2024/25 kuzalisha sukari ya kutosheleza Watanzania pia na ziada kuuzwa nje ya nchi

Aidha,Mhe Bashungwa alihaidi kukutana na Wizara ya Kilimo ili kuweza kuangalia uwezekano wa kurekebisha sheria na kanuni zinazozuia uzalishaji wa sukari kwa wajasiliamali wadogo kuzalisha sukari.

Maneno haya aliyasema jana tarehe 25/04/2020 alipotembelea TEMDO kwaajili ya uzinduzi wa Mashine Mpya zilizonunuliwa kwa fedha ya serikali